MAJAJI, MAHAKIMU WANAWAKE WATOA ELIMU SIKU YA KIMATAIFA YA MAJAJI, MAHAKIMU MBEYA

Katika kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu wanawake walitumia siku hiyo ya jana tarehe 10 Machi, 2025 kutoa elimu katika shule mbalimbali za Msingi na Sekondari za jiji la Mbeya.

Aidha, Shule zilizotembelewa katika zoezi hilo la utoaji elimu ni pamoja na Sangu High School, Samora Michel High School zilizopo katika Wilaya ya Mbeya na kutoa elimu kwa wanafunzi takribani 100,000 kutoka kwa waheshimiwa Majaji na Mahakimu Wanawake.

Waheshimiwa hao walitoa mada zilizoandaliwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) zenye lengo la kuelimisha umma juu ya haki za msingi katika zama za kidigitali, huku wakifafanua mchango wa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kushughulikia makosa ya unyanyasaji wa kimtandao kwa jinsia zote.

Waheshimiwa waliyoshiriki kutoa elimu hiyo walikuwa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Atuganile Ngwala, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe Zawadi Laizer, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mwanjelwa Mhe. Angela Kannyaninyi Byera, Mhe. Joyce Massawe, Hakimu mkazi mahakama ya Mwanzo Mwanjelwa, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Iyunga Mhe. Hafsa Shelimo na Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini Mhe. Miriam Kamwaga.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved