Activities

Wana-TAWJA (Tanzania Women Judges Association) walishiriki katika side event ya MOCLA iliyokuwa na kichwa cha habari: “Kuimarisha Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana. Huduma za Misaada ya Kisheria katika Kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia na Kuwawezesha Wanawake”.
The Minister for Community Development, Gender, Women and Special Groups, Dorothy Gwajima, has said the effective use of technology in court systems can significantly strengthen access to justice for women and girls, particularly survivors of gender-based violence.
Mkutano huo ni wa 70 kuhusu Hali ya Wanawake Duniani unaoongozwa na Kaulimbiu isemayo “Kuhakikisha na Kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana wote, ikiwa ni pamoja na kukuza mifumo ya kisheria nyenye usawa na jumuishi, kuondoa sheria, sera, na desturi za kibaguzi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo”, (Ensuring and Strengthening access to justice for all Women and Girls, including by promoting inclusive and equitable legal system, eliminating discriminatory laws, policies, and practices and addressing structural barriers”).
Kongamano maalumu la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu Wanawake limefanyika Machi 10, 2026 katika ukumbi wa New Generation jijini Dodoma.
Mbeya zone walifanya Mootcourt na wanachuo wa CUoM Mbeya, Geni Rasmi alikuwa Mhe.Jaji Joachim Tiganga J I/c Mbeya Zone, Kupinga ukatili wa kijinsia
Kongamano hilo lilifanyika Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa Mama Mariam Mwinyi, Mke wa Rais wa Zanzibar
Katika picha viongozi wa TAWJA -EXCOM Leo wamefanya mazungumzo na Wizara ya Katiba Na Sheria mjini Dodoma kuhusu kuwa na ushirikiano wa kutoa elimu kwa umma.
Wana TAWJA Kanda ya Lindi wilayani Ruangwa wakitoa elimu katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mahakama ya mwanzo Ruangwa
TAWJA Tabora kwa kushirikiana na dawati la jinsia, polisi leo tarehe 25/11/2025 wametoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia mtandaoni, katika kituo cha Redio Uyui FM-Tabora.
Wana Tawja Dodoma, Mhe Juliana Mvungi na Mhe Nyamizi Kafuku wakishiriki katika ufunguzi wa kampeni za siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mhe. Fatma H ,J na Mhe. Nayla Wana TAWJA Kanda ya Zanzibar wakitoa elimu katika TV ya Taifa ZBC kwenye siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mafunzo haya yalifunguliwa 23/10/2025 Dodoma na Mhe George Masaju Jaji Mkuu wa Tanzania, mafunzo haya yanaendelea na mada mbalimbali zinawasilishwa kwa siku mbili
Mhe George Mcheche Masaju, Jaji Mkuu wa Tanzania akizungumza na viongozi wa TAWJA katika ofisi yake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania- Dodoma
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Mhe. Barke Sehel amesema kuwa ofisi ya Makao Makuu ya chama hicho kwa sasa imehamia rasmi mkoani Dodoma.
Mkutano wa 17 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) umehitimishwa huku wanachama wa Chama hicho wakisisitizwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu. Akifunga mkutano huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwakilishi wa Jaji Mkuu wa Afrika Kusini ambaye ni Jaji wa Mahakama Kikatiba ya Nchi hiyo, Mhe. Nonkosi Mhlantla aliwataka washiriki wa mkutano huo kujithamini na kujipenda sambamba na kutosahau waliyojifunza wakati wote wa mkutano huo.
umla ya Majaji na Mahakimu Wanawake 43 ambao ni wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wamewasili katika Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini leo tarehe 08 Aprili, 2025 kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 17 wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (IAWJ) unaotarajiwa kuanza kesho tarehe 09 Aprili, 2025.
Today, as we celebrate the International Day of Women Judges, I am pleased to share an article that showcases the remarkable journeys of some inspiring women judges from Canada, El Salvador, the Republic of Korea, and a Deputy Registrar from the United Republic of Tanzania.
Katika kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu wanawake walitumia siku hiyo ya jana tarehe 10 Machi, 2025 kutoa elimu katika shule mbalimbali za Msingi na Sekondari za jiji la Mbeya.
Mwenyekiti wa TAWJA pamoja na wanachama wakiwa katika banda la TAWJA Dodoma katika uzinduzi wa wiki ya sheria
Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Dodoma na Morogoro wamepongeza Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Latifa Alhinai Mansoor baada ya kuapishwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Januari, 2025.
Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) leo tarehe 19 Januari, 2025 kimefanya mbio maalum zilizohusisha Majaji, Naibu Wasajili, Mahakimu, vikundi vya riadha pamoja na Wadau mbalimbali ili kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.
Majaji na Mahakimu Wanawake wa Mahakama ya Tanzania wanatarajia kuungana na Majaji wanawake wenzao kutoka Ukanda wa Afrika kushiriki katika Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (IAWJ) utakaofanyika jijini Accra nchini Ghana.
TAWJA discussed in detail the theme on “women in justice: examining judicial stress & gender role” (mwanamke katika utoaji haki: Tafakuri ya msongo wa mawazo na majukumu ya kijinsia).
On 28th day of October 2011, Her Excellency the President of United Republic Tanzania, Samia Suluhu Hassan launch the country’s first Gender Bench Book on women’s rights. The gender Bench Book was developed by TAWJA in collaboration with UN Women Tanzania. The aim of the book is to provide an accessible user friendly reference guide for judicial officers in protecting the rights of the women and children.
Year 2009 to 2011: The Millennium Development Goal 3 Project: (MDG 3 Project). The MDG3 Project is generously funded by the Royal Government of the Netherland for Tanzania, Bosnia Herzegovina and the Philippines.
Under the JOG Program, TAWJA networked with the Society for Women against AIDS in Tanzania (SWAA-T) which has Community Based Organizations (CBOs) in twenty districts in the country. TAWJA conducted a Training of Trainers Workshop at Arusha for SWAA-T’s CBOs’ leaders to empower them to train other leaders and members in human rights laws with a view to disseminate elementary human rights knowledge and skills to grass root level.
Training of Trainers Workshop for Judges: 21st March to 1st April, 2011 To enable more Judges and Magistrates to get human rights training under JOG, the United Nations Women Organisation (UN WOMEN) funded a Trainers Workshop (TOT) for 14 judges, and Registrars at Arusha.
JOG was essentially an extension of JEP but under a different name because donors have different names. JOG was kindly funded by the United Nations Democracy Fund (UNDEF) through the International Association of Women Judges (IAWJ) as the implementing organisation.
The International Association of Women Judges jointly with the Tanzania Women Judges Association, and with the generous sponsorship of the United Nations Women Organisation (UNIFEM), now UN WOMEN, initiated and executed the Jurisprudence of Equality Program.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved