Month: March 2026

Wana-TAWJA (Tanzania Women Judges Association) walishiriki katika side event ya MOCLA

Wana-TAWJA (Tanzania Women Judges Association) walishiriki katika side event ya MOCLA

Wana-TAWJA (Tanzania Women Judges Association) walishiriki katika side event ya MOCLA iliyokuwa na kichwa cha habari: “Kuimarisha Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana. Huduma za Misaada ya Kisheria katika Kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia na Kuwawezesha Wanawake”.

Katika side event hiyo, Mhe. Barke Sehel Jr., Mwenyekiti wa TAWJA, ndio aliyefungua, na ilifungwa na Mhe. Sauda Mjasiri (Rtd J).

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

TAWJA members who participated in the CSW New York conference in a group photo with Hon. Gwajima, Minister for Women, Gender and Community Development

TAWJA members who participated in the CSW New York conference in a group photo with Hon. Gwajima, Minister for Women, Gender and Community Development

Attended AU Ministerial Consultation Meeting with Africa Group followed by UN Women on 13 March, 2026. The objective of the meeting were to reflect on streghthening Africa’s voice at CSW, receive update on the negotiations and exchange views on Africa’s candidancy to host the first regional rotation during CSW74 to be held in 2030.

Members discussed and observed that:
1. Gender norms are regressing
2. ⁠Africa has diverse issues need to be addressed strategically and come up with one voice
3. Negotiators managed to foster for family issues, education, right to development and technical support. Other issues could not be agreed upon even within the member states. They were divided which made negotiators’ task difficult.
4. ⁠UN Women extended its support for the Africa candidacy to host CSW74 whereby in November, 2026 a preparatory meeting will be held.
5. ⁠African Women Convention on Ending Violence Against Women received few signatories. Member states are finalizing internal procedures to ratify it.
It was resolved that:
1. In order to strengthen common position, CSW Bureau should include negotiators and members from Africa at all stages, nationally and internationally.
2. ⁠Africa should hold firm on what have been achieved from Beijing Platform and it should be used as a reference point.
3. ⁠Members States should swiftly ratify the Convention
4. ⁠Strong Alliance and Strategic communications backed up with data should be used to monitor progress made so far.
5. A request for Ministers to attend national IDW will be taken up by the Bureau for action.
6. ⁠Information should be availed to members as to what entails in hosting CSW74.
7. ⁠CSW should continue to use technology in hosting its meetings to allow wider participation.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

NCHI WANACHAMA UMOJA WA MATAIFA WAKUTANA KUJADILI HALI YA WANAWAKE DUNIANI.

NCHI WANACHAMA UMOJA WA MATAIFA WAKUTANA KUJADILI HALI YA WANAWAKE DUNIANI.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekutana Jijini New York nchini Marekani kwa lengo la kujadili hali ya Wanawake katika nchi hizo.

Mkutano huo ni wa 70 kuhusu Hali ya Wanawake Duniani unaoongozwa na Kaulimbiu isemayo “Kuhakikisha na Kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana wote, ikiwa ni pamoja na kukuza mifumo ya kisheria nyenye usawa na jumuishi, kuondoa sheria, sera, na desturi za kibaguzi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo”, (Ensuring and Strengthening access to justice for all Women and Girls, including by promoting inclusive and equitable legal system, eliminating discriminatory laws, policies, and practices and addressing structural barriers”).

Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Machi 09, 2026 na utamalizika Machi 19, 2026.

Mkutano utajadili masuala mbalimbali ya upatikanaji wa haki na huduma kwa Wanawake ikiwemo haki ya upatikanaji wa Ardhi, haki kwa upatikanaji wa Elimu, haki ya kujua masuala ya sheria na upatikanaji wa haki za kisheria, kushiriki katika masuala ya uongozi na siasa, haki ya kumilili na upatikanaji wa huduma bora za Afya.

Siku ya kwanza ya mkutano huo, Tanzania imeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu, Wataalamu kutoka Wizara hiyo, Wizara nyingine za Kisekta, Taasisi za Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Aidha taarifa ya Nchi katika Mkutano huo itatolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Kongamano maalumu la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu Wanawake

Kongamano maalumu la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu Wanawake

Kongamano maalumu la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majaji na Mahakimu Wanawake limefanyika Machi 10, 2026 katika ukumbi wa New Generation jijini Dodoma, likiwakutanisha viongozi wa Serikali, Mahakama ya Tanzania na wadau wa maendeleo kujadili nafasi ya wanawake katika sekta ya utoaji haki na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Jaji wa Mahakama ya Rufani Rehema Joseph Kerefu alisema kuwa majaji na mahakimu wanawake wana nafasi muhimu katika kuimarisha utoaji wa haki unaozingatia usawa wa kijinsia na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea kujitokeza katika jamii.

Alieleza kuwa licha ya kuwepo kwa misingi ya kisheria na kitaaluma inayolinda haki za wanawake, bado baadhi ya mila na desturi zinazochochea mfumo dume zimekuwa kikwazo katika kufanikisha usawa wa kijinsia, huku changamoto kama ubakaji, unyanyasaji wa kingono, ukatili wa majumbani na ndoa za utotoni zikiendelea kujitokeza.

Washiriki wa kongamano hilo pia walibainisha kuwa Tanzania imepiga hatua katika kuongeza uwakilishi wa wanawake katika Mahakama, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kutumia nafasi hizo kuimarisha utoaji wa haki na kuongoza mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved