Author: admin

TAWJA -EXCOM wafanya mazungumzo na Wizara ya Katiba Na Sheria mjini Dodoma

TAWJA -EXCOM wafanya mazungumzo na Wizara ya Katiba Na Sheria mjini Dodoma

Katika picha viongozi wa TAWJA -EXCOM Leo wamefanya mazungumzo na Wizara ya Katiba Na Sheria mjini Dodoma kuhusu kuwa na ushirikiano wa kutoa elimu kwa umma na kujrnga uwezo kwa Majaji na Mahakimu Wanawake na hasa katika kuashimisha siku ya kimataifa ya Majaji na Mahakimu Wanawake duniani.

Mwenyekiti huyo ameeleza kwamba, katika Mkutano huo, Mahakama ya Tanzania itapata nafasi ya kutoa mada ya kuelezea hatua zinazochukuliwa na TAWJA katika kumpa nafasi mwanamke kwenye Uongozi hasa kwenye Mahakama.

Kaulimbiu ya Mkutano huo inasema ‘Nafasi ya Majaji Wanawake katika kupambana na mila potofu katika ulimwengu wa sasa.’

Mbali na TAWJA, Vyama vingine vitakavyoshiriki katika mkutano huo ni kutoka Nigeria, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Cote d’Ivoire na nyingine.

Kiongozi wa msafara wa wanachama wa TAWJA, Mhe. Sehel pamoja na wenzake wamewasili leo hii jijini Accra majira ya saa 5 asubuhi tayari kwa kushiriki kikamilifu Mkutano huo muhimu.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Wana TAWJA Kanda ya Lindi wilayani Ruangwa

Wana TAWJA Kanda ya Lindi wilayani Ruangwa

Wana TAWJA Kanda ya Lindi wilayani Ruangwa wakitoa elimu katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mahakama ya mwanzo Ruangwa

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Wana TAWJA Tabora katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 

Wana TAWJA Tabora katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 

TAWJA Tabora kwa kushirikiana na dawati la jinsia, polisi leo tarehe 25/11/2025 wametoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia mtandaoni, katika kituo cha Redio Uyui FM-Tabora.
Hii ni katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Katika picha ni Mhe Monika Muhandikila & Mhe Paulina Mkaumbya.

Mwenyekiti huyo ameeleza kwamba, katika Mkutano huo, Mahakama ya Tanzania itapata nafasi ya kutoa mada ya kuelezea hatua zinazochukuliwa na TAWJA katika kumpa nafasi mwanamke kwenye Uongozi hasa kwenye Mahakama.

Kaulimbiu ya Mkutano huo inasema ‘Nafasi ya Majaji Wanawake katika kupambana na mila potofu katika ulimwengu wa sasa.’

Mbali na TAWJA, Vyama vingine vitakavyoshiriki katika mkutano huo ni kutoka Nigeria, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Cote d’Ivoire na nyingine.

Kiongozi wa msafara wa wanachama wa TAWJA, Mhe. Sehel pamoja na wenzake wamewasili leo hii jijini Accra majira ya saa 5 asubuhi tayari kwa kushiriki kikamilifu Mkutano huo muhimu.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Wana Tawja Dodoma katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wana Tawja Dodoma katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wana Tawja Dodoma, Mhe Juliana Mvungi na Mhe Nyamizi Kafuku wakishiriki katika ufunguzi wa kampeni za siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, yaliyofanyika katika kata ya Handali Wilayani Chamwino Dodoma , leo tarehe 25 Nov, 2025

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Wana TAWJA Zanzibar katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia TAWJA leading the way

Wana TAWJA Zanzibar katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia TAWJA leading the way

Mhe. Fatma H ,J na Mhe. Nayla Wana TAWJA Kanda ya Zanzibar wakitoa elimu katika TV ya Taifa ZBC kwenye siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Ufunguzi wa Mafunzo ya waratibu wa TAWJA kutoka kila mkoa.

Ufunguzi wa Mafunzo ya waratibu wa TAWJA kutoka kila mkoa.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju amesema Majaji na Mahakimu Wanawake nchini wana wajibu mkubwa wa kusimamia haki za binadamu, maadili ya jamii na usawa wa kijinsia ili kuleta ustawi katika jamii.

Akizungumza jana tarehe 23 Oktoba, 2025 wakati akifungua Mafunzo kwa Waratibu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) kwenye ukumbi wa Mikutnao wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Mhe. Masaju alisema kupitia mafunzo hayo ni muhimu wakaweka mikakati thabiti itakayowezesha kufikia ustawi katika jamii.

“Ninachoona ni kwamba ninyi TAWJA mnajitambua, wajibu wenu leo ni kuja na mikakati ambayo itawezesha kutatua hizi changamoto ambazo zimekuwa zinajitokeza kwenye haya masuala yanayowahusu na hasa haki za binadamu wote ambao humo wanajumuishwa Wanawake na Wanaume wakiwa wa umri mbalimbali, wengine watu wazima, wengine wazee na wengine Watoto kwa mfano kuna changamoto hii ya makosa unyanyasaji wa kijinsia,” alisema Jaji Mkuu.

Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) jana tarehe 23 Oktoba 2025 kimeanza kufanya mafunzo maalum kwa Waratibu wa Kikanda wa chama hicho, ambayo yamelenga kuimarisha uongozi, usimamizi na uwajibikaji katika kulinda haki za kijinsia na za binadamu.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, ambapo mgeni rasmi alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa TAWJA ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Barke Sehel, alisema kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo kuongeza uwezo wa Waratibu wa Mkoa katika uratibu, mawasiliano, na utekelezaji wa programu za kikanda.

“Tunatarajia kuwa kupitia waratibu hawa, TAWJA itaimarika na kuwa kinara katika ulinzi wa haki za binadamu na usawa wa kijinsia nchini,” alisema Mhe. Sehel.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

Mhe George Mcheche Masaju, Jaji Mkuu wa Tanzania akizungumza na viongozi wa TAWJA

MAKAO MAKUU YA TAWJA RASMI DODOMA

MAKAO MAKUU YA TAWJA RASMI DODOMA

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Mhe. Barke Sehel amesema kuwa ofisi ya Makao Makuu ya chama hicho kwa sasa imehamia rasmi mkoani Dodoma.

Akiongoza kikao hivi karibuni cha wanachama wa TAWJA wa mkoani humo kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma, Mhe. Sehel alisema kuwa, hatua ya kuhamia Dodoma kutarahisisha mawasiliano, kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi lakini pia kukuza utendaji wa kisekta ndani ya mfumo wa haki nchini.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa neema yake ya kutufanya leo tumekutana hapa Dodoma na kuzungumza na wenzangu lakini pia nitumie fursa hii kuwajulisha kuwa kuanzia sasa ofisi ya TAWJA rasmi imehamia Dodoma na itakuwa katika Jengo la Makao Makuu ya Mahakama,” alisema Mhe. Sehel.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma ambaye pia ni Mlezi wa Chama hicho kwa Kanda hiyo, Mhe. Dkt. Juliana Masabo aliwapongeza wanachama wote na kuwakaribisha wanachama wengine katika Mkoa wa Dodoma na kuahidi kushirikiana nao kwa kila kitu.

Nao Wajumbe wa TAWJA Kanda ya Dodoma, walipongeza juhudi za viongozi wa chama hicho kwamba, hatua hiyo italeta fursa mpya katika kushirikiana, kuongeza ufanisi na maendeleo katika mfumo wa utoaji haki pamoja na shughuli nyingine za kijamii.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi kutoka Mahakama ya Rufani ambao ni Majaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa TAWJA Taifa, Mhe. Barke Sehel, Mhe Patricia Fikirini, Mhe. Lucy Kairo, Mhe. Zainab Muruke, Mhe Leila Mgonya pamoja na viongozi wengine wanawake kutoka Mahakama.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

MKUTANO WA 17 WA IAWJ WAHITIMISHWA

MKUTANO WA 17 WA IAWJ WAHITIMISHWA

Mkutano wa 17 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) umehitimishwa huku wanachama wa Chama hicho wakisisitizwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.

Akifunga mkutano huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwakilishi wa Jaji Mkuu wa Afrika Kusini ambaye ni Jaji wa Mahakama Kikatiba ya Nchi hiyo, Mhe. Nonkosi Mhlantla aliwataka washiriki wa mkutano huo kujithamini na kujipenda sambamba na kutosahau waliyojifunza wakati wote wa mkutano huo.

“Nawasihi kutosahau kupitia mliyojifunza mtapata uzoefu mzuri, Majaji mbalimbali walipata nafasi ya kuchangia uzoefu wao juu ya namna wanavyoshughulikia mashauri yanayohusu vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ya wanawake, hivyo ni muhimu kujifunza na kuyaishi yote mazuri tuliyoyapata,” alisema Mhe. Mhlantla.

Jaji huyo aliwakumbusha Majaji na Mahakimu wanawake kujipenda na kujithamini kwanza ambapo alisema, “ni muhimu kujipenda na kujithamini, kufanya hivyo sio ubinafsi bali ni muhimu kufanya hivyo ili tuwe katika nafasi nzuri ya kutekeleza vizuri majukumu yetu ipasavyo,” alisisitiza.

Aidha, Jaji Mhlantla  alisema kuwa, bado Mahakama nyingi hazina mbinu za kiusalama katika kuwalinda wahanga wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia huku na kusema kwamba kuna haja ya kuchukua hatua thabiti ili kuwalinda watu hao.

Mgeni Rasmi huyo alizikumbusha pia nchi wanachama wa IAWJ kufanya uanaharakati ndani ya Mahakama hususani unaohusiana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hususani akili unde ili kushughulikia matatizo mbalimbali yaliyopo ndani ya Mahakama ambayo ni pamoja na mlundikano wa mashauri.

Wakati wa mkutano huo uliofanyika kwa siku nne mada mbalimbali ziliwasilishwa ambazo ni pamoja na Majaji wanawake wanaongoza kuleta mabadiliko katika Mahakama za Kimataifa, Wanawake katika Uongozi-Mahali pa Kazi Usalama kwa Maafisa wa Mahakama, Ubaguzi na biashara haramu ya binadamu na nyingine.

Mada nyingine iliwasilishwa na Mhe. Edith Mwalukasa, Hakimu kutoka Mahakama ya Mwanzo Bagamoyo Tanzania mada hiyo ilijikita kuzungumzia ‘Athari za teknolojia katika masuala ya ukatili wa kijinsia.’ 

Aidha, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama hicho, wanachama wa IAWJ walifanya uchaguzi na kumchagua Rais mpya wa Chama hicho ambaye ni Mhe. Maria Filomena D. Singh kutoka nchini Morocco.

Mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili umeazimia kuwa, Mkutano ujao wa mwaka 2027 utafanyikia nchini Canada.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved

TAWJA YAWASILI CAPE TOWN KUSHIRIKI MKUTANO MKUU WA MAJAJI WANAWAKE DUNIANI

TAWJA YAWASILI CAPE TOWN KUSHIRIKI MKUTANO MKUU WA MAJAJI WANAWAKE DUNIANI

Jumla ya Majaji na Mahakimu Wanawake 43 ambao ni wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wamewasili katika Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini leo tarehe 08 Aprili, 2025 kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 17 wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (IAWJ) unaotarajiwa kuanza kesho tarehe 09 Aprili, 2025.
Akizungumza katika mahojiano maalum leo tarehe 08 Aprili, 2025 mjini humo, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Mhe. Barke Sehel amesema kuwa, Mkutano huo unatarajiwa kuanza rasmi kesho tarehe 09 hadi 12 Aprili, 2025 na Mgeni Rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa.
“Mkutano huu ni wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Duniani, kwa ujumla unawakutanisha wanachama Majaji na Mahakimu wanawake duniani. Kwa upande wa Tanzania tutakaoshiriki katika Mkutano huo ni wanachama 43 idadi hii imejumuisha na wenzetu wa Zanzibar,” amesema Mhe. Sehel.
Kaulimbiu ya Mkutano huo inasema; ‘Wanawake na uongozi katika kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ya dhidi ya wanawake.’
Mhe. Sehel amesema kuwa, mada mbalimbali zitawasilishwa katika mkutano huo ni pamoja na Majaji wanawake wanaongoza na kuleta mabadiliko katika Mahakama za Kimataifa, Wanawake katika Uongozi-Mahali pa Kazi Usalama kwa Maafisa wa Mahakama, Ubaguzi na biashara haramu ya binadamu na nyingine.
Kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano huo, mmoja wa washiriki watakaotoa mada ya ‘Athari za teknolojia katika masuala ya ukatili wa kijinsia’ ni Mhe. Edith Mwalukasa ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mwambao Bagamoyo.
Washiriki wa TAWJA wanaotarajia kuhudhuria mkutano huo ni baadhi ya wanachama ni kutoka kutoka Zanzibar, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Arusha, Tabora na Mikoa mingine ya Tanzania Bara.

Mkutano wa aina hii huwakutanisha pamoja Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani kote na hufanyika kila baada ya miaka miwili na huwapa fursa Majaji hao kujadili masuala mbalimbali yanayohusu haki za wanawake, ukatili wa kijinsia, watoto na jamii kwa ujumla.

© 2024 Tanzania Women Judges Association. All Rights Reserved